Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Gennadi Gatilov
Urusi kwa mara nyingine imeuonya utawala haramu wa Israel kuhusu maafa makubwa yatakayojiri iwapo utawala huo utathubutu kuishambulia kijeshi Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Gennadi Gatilov amesema mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Iran yatasababisha maafa makubwa kieneo na kimataifa.
Marekani, utawala wa Kizayuni wa Israel na waitifaki wao wamekuwa wakiituhumu Iran kuwa ina malengo ya kijeshi katika mpango wake wa nyukla. Kwa kisingizio hicho wamekuwa wakitoa vitisho vya kuishambulia Iran kijeshi.
Iran inasisitiza kuwa shughuli zake za nyuklia zinafanyika kwa malengo ya amani. Aidha Iran inasema kwa vile ni mwanachama wa Mkataba wa Kuzuia Utengenezaji na Usambazaji Silaha za Nyuklia NPT na vile vile kama mwanachama wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA ina haki ya kutumia teknolojia ya nyuklia kwa malengo ya amani.
No comments:
Post a Comment