Your help needed

As we committed ourselves to have our own premises for an improvement and to provide high quality of Islam education for the muslims in Leicester, Madrasatul Noor Leicester would like to take an oppertunity to inform every one who wish to contribute and to support our project to use our account below: Madrassatul Noor Leicester Lloyds TSB Bank Account number: 45127768 Sort Code: 30-94-97 International Bank account: LOYDGB21029 GB27LOYD30949745127768 If you would like to have more information please do not hasitate to contact us through these emails: madrasatulnoor.01@gmail.com or fcalwattan@gmail.com With a lot of thanks

23 Apr 2016

Our new community website

We are pleased to announce the launch of our new website. Please click here to check it out!

All updates will be posted in the new website. Thank you.

28 Jan 2015

Msaada wa ujenzi wa Msikiti Mafia

Wakaazi wa Mafia na baadhi ya vitongoji vyake wanawaomba waislamu wote popote pale duiniani kusaidia ujenzi wa msikiti mpya ambao tayari umeshakuwa upo katika harakati za ujenzi.

Kwa maelezo zaidi na namna gani jinsi ya kusaidia tafadhali wasiliana na Bwana Juma Yakoub kwa namba hii: +255 687 570799.

Tukumbuke kuwa Mtume Muhammad (SAW) amesema "Yeyote atakaejenga msikiti kwa ajili ya Allah, basi Allah nae atamjengea nyumba peponi".

Zifuatazao ni picha za msikiti uliopo sasa na picha za jengo jipya:

 
Huu ndio msikiti utumikao kwa sasa

Maendeleo ya jengo jipya la msikiti

15 Jan 2015

Msiba katika mji wa Leicester UK

Ndugu Hussein Issa Mohammed wa mjini Leicester anatangaza msiba wa kifo cha mwanawe wa kumzaa Abubakar Hussein kilichotoke siku ya Jumatatu kwa ajali ya gari.

Mipango ya mazishi bado inaendelea na habari kamili zikishapatikana tutawajulisha.

Tumuombe Allah amsamehe madhambi yake ya siri na ya Dhahiri, amuondoshee adhabu ya kaburi na amjaalie awe katika waja wa peponi.

Ameen

25 Sept 2014

Tangazo la Sala ya Eid Al Hajj Leicester


Asalaam aleykum, An Noor Community Centre wakishirikiana na Madrasatul Noor Leicester wanawajulisha waislamu wote ya kuwa panapo majaaliwa sala Eid Al Hajj itasaliwa siku ya Jumamosi tarehe 4 October 2014 hapo katika msikiti wa An Noor Leicester. Takbeer zitaanza saa mbili na robo asububuhi (08.15 am) na sala itasaliwa saa mbili na nusu (08.30 am).

Kama kawaida wanaume watakuwa eneo la chini na wanawake wao watakuwa eneo la juu. Tafadhali jitahidi kufika mapema.
Shukran

Taarifa ya muandamo wa mwezi wa Dhul Hijja, siku ya Arafah na siku ya Eid

As-Salaamu 'Alaykum wa RahmatuLLaah wa Barakaatuh
Tunapenda kuwaatarifu kwamba mwezi wa Dhul-Hijjah umeandama na hivyo siku ya Alkhamis ni mwezi 1 Dhul-Hijjah 1435 (25 Septemba 2014) na ‘Arafah itakuwa ni Siku ya Ijumaa  mwezi 9 Dhul-Hijjah (3 Oktoba 2014) na ‘Eidul-Adhw-haa itakuwa ni Jumamosi mwezi 10 Dhul-Hijjah (4 Oktoba 2014)).
Kadhaalika tunapenda kuwakumbusha ndugu zetu mambo mawili muhimu  tunayoghafilika nayo katika masiku ya Dhul-Hijjah
Kuchinja: Wenye  kunuia kuchinja au kuchinjiwa, wanatakiwa wajizuie kukata nywele na kucha kuanzia unapoingia tu mwezi wa Dhul-Hijjah mpaka watakapomaliza kuchinja. Haya ni maamrisho yanayopatikana katika Hadiyth ifuatayo:
عن أم سلمة رضي الله عنها، أن النبي صلى الله عليه وسلم قال: (((ِذَا رَأَيْتُمْ هِلَالَ ذِي الْحِجَّةِ وَأَرَادَ أَحَدُكُمْ أَنْ يُضَحِّيَ ، فَلْيُمْسِكْ عَنْ شَعْرِهِ وَأَظْفَارِهِ))) وفي راوية: ((فَلَا يَأْخُذْ مِنْ شَعْرِهِ وَلَا مِنْ أَظْفَارِهِ شَيْئًا ، حَتَّى يُضَحِّيَ)) مسلم
Imetoka kwa Ummu Salamah (Radhiya Allaahu 'anha) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Ukiandama mwezi wa Dhul-Hijjah na ikiwa yuko anayetaka kuchinja basi azuie (asikate) nywele zake na kucha zake) Na katika riwaya nyingine ((Asikate nywele wala kucha mpaka akimaliza kuchinja)) [Muslim na wengineo]
 Source: Alhidaaya

11 Sept 2014

Documentary: British women are converting to Islam


Tangazo la Muhadhara Leicester Uingereza



Asalaam Aleykum,

Ndugu zangu katika IMANI, An Noor Community Centre wakishirikiana na Madrassatul Noor Leicester kwa pamoja wanakualika muhadhara wa dini ya kiislamu utakaofanyika siku ya Jumamosi ya tarehe 27/09/2014, katika msikiti wa An Noor kuanzia saa kumi kamili jioni (4pm).

Muhadhir mkuu atakuwa Sheikh Nassor kutoka London.

Waislamu wote wa kike na wa kiume wanakaribishwa. Wanawake nafasi yao itakuwa eneo la juu ya msikiti.

Tafadhali jitahidi kuisambaza habari hii ya muhadhara kwa waislamu wengine.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na:
Abdul Dau: 07792104495
Ustadh Farid: 07792174408
Ustadh Issa: 07984106983

Anuani kamili ya msikiti ni:
170a Belgrave Gate
Leicester
LE1 3XL

Wabillah Tawfiq

27 Jul 2014

Sala ya Eid Leicester


An Noor Community Leicester Inapenda kuwatangazia waislamu wote ya kuwa Sala ya Eid itaswaliwa katika msikiti wa An Noor sa mbili na nusu asubuhi (08:30 am).

Anuani kamili:
170a Belgrave Gate
Leicester
LE1 3XL

Kutakuwa na kifunguwa kinywa cha pamoja mara tu baada ya kukamilika kwa sala ya Eid


Wabillah Tawfiq

8 Jul 2014

Safari ya Umrah mwaka 2015 kwa wakazi wa Uingereza



Kampuni ya Mreh Tours ikishirikiana na Alsharif Tours zote za jijini la Leicester nchini Uingereza zimewaandalia 'OFFER' maalum ya safari ya Umrah mwaka 2015 kwa wakazi wa Uingereza.

Gharama za safari hiyo ni £1000, ambayo ni nauli ya kwenda na kurudi Saudi Arabia, Visa, hotel (usiku tano Madina na usiku tano Makkah), Chakula (mara tatu kwa siku), safari za ndani ya miji ya kiislamu, Ihram na Sim card ya kutumia Saudia.

Safari hiyo ambayo ina lengo kwa vijana wa kiume wenye umri kuanzia miaka 13, lakini pia hata kwa watu wazima ambao watakuwa wanataka kujumuika katika safari hiyo pia nafasi zinapatikanwa.

Tafadhali wasiliana na wahusika mapema ili uwahi kuweka nafasi yako mapema kabla ya nafasi hizo kujaa.

Wasiliana na:
Mreh: 07931417575
Khalfan: 07861499751
Sharif: 07951315110

5 Jul 2014

Picha: PBZ yafutarisha wateja wake Pemba

 MAKAMO wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe:Maalim Seif Sharif Hamad, akisalimiana na viongozi wa Benk ya watu wa Zanzibar, PBZ Tawi la Pemba wakati alipokuwa akiwasili katika futari maalumu iliyoandaliwa na Benk hiyo kwa wateja wake huko ZSSF Chake Chake Pemba.
 
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa na Viongozi wa Serekali na wa PBZ, wakati wa futari Maalum ilioandaliwa na Benki ya Watu wa Zanzibar Ltd, kwa Wateja wake Kisiwani Pemba, iliofanyika katika viwanja vya Hoteli ya ZSSF Chakechake Pemba jana.
 
 Wananchi na Wafanyabiashara Kisiwani Pemba wakipata futari maalum ilioandaliwa na PBZ kwa ajili ya Wateja wao walioko Pemba na kujumuika na Wafanyakazi wa PBZ Tawi la Pemba, futari hiyo imefanyika katika viwanja vya hoteli ya ZSSF Chakechake Pemba jana. 
 
Wananchi wakipata futari maalum iliandaliwa na PBZ Tawi la Pemba katika viwanja vya hoteli ya ZSSF Pemba.
 
Mkurugenzi Mtendajin wa Benki ya Watu wa Zanzibar Ndg Juma Amour, akitowa shukrani kwa Wananchi na Wafanyabiasha wa Kisiwani Pemba baada ya kumaliza kupata futari ilioandaliwa kwa ajili yao katika viwanja vya hoteli ya ZSSF Chake Pemba na kuhudhuriwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad.(Picha na Abdi Suleiman -Pemba)  

Chanzo: Zanzinews

Picha: Masjid Huda ya Chamazi Mbagala Dar yafunguliwa rasmini na Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi

Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya SSB. Ndg. Said Salim Bakressa.
 
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na Rais Mstaaf wa Tanzania Alhajj Ali Hassan Mwinyi,alipowasili viwanja vya Masjid Huda Mbagala Chamazi kwa ajili ya Uzinduzi wa Masjid Huda. 


Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, akikata utepe kuzindua rasmi Msikiti wa ‘Masjidil Huda’ uliojengwa na mfanyabiashara maarufu nchini, Said Salim Bakhresa  katika eneo la Uwanja wa Chamazi, Mbagala jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti huyo wa Makampuni ya SSB, Said Salim Bakhresa, ambapo pia uzinduzi huo uliofanyika leo Julai 4, 2014, ulihudhuriwa na baadhi ya Viongozi wa Kiserikali akiwemo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na wengineo.
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (wa tatu kulia) Rais Mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi (wa pili kushoto) Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana ( wa pili kulia) Mwenyekiti wa Makampuni ya SSB, Said Salim Bakhresa (katikati) na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum (kushoto) wakijumuika na waumini wa dini ya Kiislam, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mkititi wa ‘Masjid Huda’ na Swala ya Ijumaa uliofanyika leo Julai 4, 2014, Chamaz jijini Dar es Salaam.