Your help needed

As we committed ourselves to have our own premises for an improvement and to provide high quality of Islam education for the muslims in Leicester, Madrasatul Noor Leicester would like to take an oppertunity to inform every one who wish to contribute and to support our project to use our account below: Madrassatul Noor Leicester Lloyds TSB Bank Account number: 45127768 Sort Code: 30-94-97 International Bank account: LOYDGB21029 GB27LOYD30949745127768 If you would like to have more information please do not hasitate to contact us through these emails: madrasatulnoor.01@gmail.com or fcalwattan@gmail.com With a lot of thanks

23 Feb 2012

Balozi Seif afungua jengo la Madrasa Hidayatul Islamiyah


Makamu wa pili wa Rais akikagua moja ya jeongo la Madrasa Hidayatul Islamia

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema ipo haja kwa Washirika na Wafadhili wa Maendeleo katika nyanja za Elimu ya Dini ndani na nje ya Nchi kufikiria zaidi wazo la kuongeza nguvu katika ujenzi wa Vyuo na Madrasa ili kuwajengea mazingira bora ya Kitaaluma watoto wa Taifa hili.

Kauli hiyo ameitoa mara baada ya kulifunguwa Jengo Jipya la Madrasa Hidayatul Islamia iliyopo Njia Kuu Moga ndani ya Wadi ya Gamba Wilaya ya Kaskazini A.

Balozi Seif alisema Jamii ya Kiislamu imeshuhudia ongezeko kubwa la Ujenzi wa Misikiti Nchini kasi ambayo inaweza pia kuelekezwa katika Vyuo na Madrasa ambayo Maeneo mengi yamekuwa na ufinyu wa Majengo hao ya Kudumu.

“ Sisemi kwamba Wafadhili wasijenge Misikiti la hasha. Lakini ni vyema kwa wafadhili wakaangalia mazingira ya Vyuo na Madrasa nyingi Nchini ambazo ama ni mbovu au hazina hadhi ya kusomeshea kitabu cha Mwenyezi Muungu ”. Alishauri na Kusisitiza Balozi Seif.

Makamu wa Pili wa Rais waZanzibaralimpongeza Mfadhili wa Madrasda hiyo Ukti Asia Mohd wa Oman kwa juhudi zake za kusaidia kupanua Elimu ya Dini Hapa Nchini.

“ Nimevutiwa na Madrasa hii. Nilipoikagua ndani nimeona Darasa la Watu Wazima. Hii ni ishara na fursa nzuri kwa nao kupata wasaa wa kujielimisha. Kwa kweli Madrasa zina umuhimu wa kipekee katika kutanua Elimu popote pale ”. Alifafanua Balozi Seif.

Balozi Seif aliwataka Vijana kuhakikisha wanaitafuta Elimu kwa Njia yoyote huku akiisisitiza Jumuiya inayosimamia masuala ya Elimu ya Dini Wilaya ya Kaskazini “A” { JUVMAWA } ikaendelea kuonyesha Njia bora kwa Watoto wanaowalea.


Balozi Iddi akimkabidhi mmoja ya wanfunzi kitabu

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameahidi kutoa Mchango wa Kompyuta moja kwa ajili ya Madrasa hiyo na kuutaka Uongozi wa Jimbo la Chaani, Wilaya ya Kaskazini A na Mkoa wa Kaskazini kuhakikisha changamoto zinazoikabili Madrasa hiyo zinatatuliwa.

Katika Risala ya Madrasa hiyo iliyosomwa na Ustadhi Khamis Hakim alisema Madrasa hiyo iliyoasisiwa zaidi ya miaka 80 ikiwa na Wanafunzi 500 mchanganyiko imekuwa chemchem ya kutoa walimu wanaoendelea kusomesha Madrasa tofauti Wilayani humo.

Wakati huo huo mamia ya Waumini wa Dini ya Kiislamu na Wananchi wamehudhuria Maulidi ya Uzawa wa Kiongozi wa Dini ya Kiislamu Mtume Muhammad { SAW }.

Maulidi hayo yaliandaliwa na Uongozi wa Masjid Noor Muhammad{ SAW } iliyopo Mtaa waMombasakwaChinaambapo Makamu wa Pili wa Rais waZanzibarBalozi Seif alikuwa Mgeni Rasmi kwenye Hafla hiyo.

Akitoa chakula cha moyo katika hadhara hiyo Mwanachuoni Maarufu ndani ya Mwambao waTanzaniaSheikh Sameer Zulfikar amewaasa Waumini wa Dini ya Kiislamu kutouacha Mwezi huu ukapita bila ya kusafisa nyoyo zao kwa kumtukuza Mtume Muhammad { SAW }.

No comments:

Post a Comment