Your help needed

As we committed ourselves to have our own premises for an improvement and to provide high quality of Islam education for the muslims in Leicester, Madrasatul Noor Leicester would like to take an oppertunity to inform every one who wish to contribute and to support our project to use our account below: Madrassatul Noor Leicester Lloyds TSB Bank Account number: 45127768 Sort Code: 30-94-97 International Bank account: LOYDGB21029 GB27LOYD30949745127768 If you would like to have more information please do not hasitate to contact us through these emails: madrasatulnoor.01@gmail.com or fcalwattan@gmail.com With a lot of thanks

29 Feb 2012

Injili ya kale iliyogunduliwa nchini Uturuki yaonesha utabiri wa kudhihiri Mtume Muhammad SAW



Nakala ya Injili ya miaka 1500 iliyopita na ambayo imepatikana tena katika kanisa moja nchini Uturuki baada ya kupotea kwa muda wa miaka 12, ina utabiri wa kuja Mtume wa Uislamu, Nabii Muhammad SAW baada ya Masihi Issa yaani Yesu AS.

Vyombo vya habari vimeripoti kuwa, nakala hiyo ya zamani sana ya Injili imeandikwa kwa lugha ya Kiarami na vyombo vya habari vinasema kuwa, ilikuwa imefichwa kwa muda wa miaka 12.

Tayari viongozi wa Vatican wameonesha hamu kubwa ya kuipata Injili hiyo na Papa Benedict wa 16 ametoa mwito wa kufanyiwa uchunguzi maandishi ya Injili hiyo.

Kwa upande wake, Waziri wa Utamaduni wa Uturuki, Ertuğrul Günay amesema kuwa, bei ya Injili hiyo ni dola milioni 22 za Kimarekani na kwa vile utabiri wa kuja Mtume Muhammad SAW unapatikana kwenye Injili hiyo yenye lugha ya Nabii Issa AS, ilikuwa imefichwa ili watu wasiione.

Amesema maneno yaliyomo kwenye Injili hiyo ya miaka 1500 iliyopita yanafanana sana na maneno ya Qur'ani Tukufu na kiujumla maneno yake yanakaribiana sana na mafundisho ya Uislamu.

Sehemu moja ya maneno yaliyomo kwenye Injili hiyo yanamtaja Yesu kuwa ni mwanadamu na kumnukuu Nabii huyo wa Mwenyezi Mungu akisema kuwa, Mtume atakayekuja baada yake anaitwa Muhammad. Sehemu ya maneno ya Injili hiyo ya miaka 1500 iliyopita yana maana isemayo: Kuhani mmoja alimuuliza Masihi Yesu kuhusu mtu atakayekuja kuchukua nafasi yake na Yesu akajibu: "Muhammad (SAW) ndilo jina lake lililobarikiwa, anatoka katika kizazi cha Ismail, baba yangu Mwarabu."

Waziri wa Utamaduni wa Uturuki pia amesema, tayari Papa Benedict wa 16 ametuma maombi rasmi ya kutaka wapatiwe Injili hiyo iliyopatikana kwenye visiwa vya Uturuki vilivyoko kwenye bahari ya Mediterranean. Imeelezwa kuwa watu waliopatikana na Injili hiyo walikuwa wana nia ya kuiuza kimagendo na hivi sasa wanashikiliwa katika mahakama za Uturuki.

Wakati huo huo kasisi Ihsan Uzbek, mmoja wa viongozi waandamizi wa Kikristo nchini Urutuki amesema kuwa Injili hiyo ni ya zama za mtakatifu Barnaba aliyeishi na Nabii Issa na ambaye alikuwa mfuasi wake wa karibu.

Huko nchini Uturuki nako kumetolewa mwito wa kufanyika uchunguzi wa kitaalamu wa kuweza kujua tarehe hasa ilipoandikwa Injili hiyo.

No comments:

Post a Comment