Your help needed

As we committed ourselves to have our own premises for an improvement and to provide high quality of Islam education for the muslims in Leicester, Madrasatul Noor Leicester would like to take an oppertunity to inform every one who wish to contribute and to support our project to use our account below: Madrassatul Noor Leicester Lloyds TSB Bank Account number: 45127768 Sort Code: 30-94-97 International Bank account: LOYDGB21029 GB27LOYD30949745127768 If you would like to have more information please do not hasitate to contact us through these emails: madrasatulnoor.01@gmail.com or fcalwattan@gmail.com With a lot of thanks

4 Jun 2012

Historia ya tarehe ya leo kiislamu (13 Rajab 1433)



Leo ni Jumatatu tarehe 13 Rajab mwaka 1433 Hijiria inayosadifina na tarehe 4 Juni 2012 Miladia
Siku kama ya leo miaka 1456 iliyopita alizaliwa Ali bin Abi Twalib katika nyumba tukufu ya al Kaaba, ambaye ni binamu, mkwe na Khalifa wa Mtume Muhammad (saw).

Mama wa mtukufu huyo ni Bibi Fatima bint Assad na baba yake ni Abu Talib. Katika kipindi chake cha utotoni, Ali bin Abi Talib alilelewa na kupata elimu na mafunzo kutoka kwa Mtume Mtukufu SAW, na alikuwa mwanaume wa kwanza baada ya Mtume SAW kuukubali Uislamu.

Mwishoni mwa mwaka wa Pili Hijria, Imam Ali AS alimuoa Bibi Fatimatul Zahra binti ya Mtume Mtukufu SAW. Imam Ali AS alishiriki kwenye vita vyote bega kwa bega na Mtume Mtukufu SAW isipokuwa vita vya Tabouk, na alikuwa msaidizi wa karibu wa Mtume Mtukufu katika hali zote za shida na matatizo.

Licha ya kuwa shujaa na mpiganaji mashuhuri, lakini Imam Ali bin Abi Twalib alikuwa mpole kwa watu wa kawaida, mwingi wa huruma na upendo na mtetezi wa wanyonge na wanaodhulumiwa. Imam Ali AS aliishi kwa muda wa miaka 63 na kwa muda wa miaka mitano ya uhai wake aliuongoza umma wa Kiislamu kama khalifa. Imam Ali AS aliuawa shahidi mwezi wa Ramadhan, baada ya kupigwa dharuba ya upanga akiwa anaswali sala ya alfajiri msikitini mjini Kufa nchini Iraq.

 Idhaa ya Kiswahili Redio Tehran inatoa mkono wa baraka na fanaka kwa Waislamu wote duniani kwa mnasaba huu adhimu wa kuadhimishwa siku ya kuzaliwa Simba wa Mungu, Imam wa Mashariki na Magharibi, Amirul Muuminin Ali bin Abi Twalib (as).

Siku kama ya leo miaka 49 iliyopita, sawa na tarehe 15 Khordad 1342 Hijria Shamsia, wananchi katika pembe mbalimbali nchini Iran walifanya maandamano makubwa dhidi ya utawala wa kifalme hapa nchini, baada ya kusambaa habari za kutiwa mbaroni Imam Khomeini. Vikosi vya usalama vya utawala wa kifalme hapa nchini vilimtia mbaroni Imam Khomeini zikiwa zimepita siku chache tu tokea alipotoa hotuba kali na ya kihistoria katika Madrasa ya Faidhiyyah mjini Qum. Harakati ya tarehe 15 Khordad inahesabiwa kuwa ndiyo chachu ya kujiri mapinduzi ya Kiislamu yaliyopelekea kuangushwa utawala wa Kipahlavi.

Na miaka 23 iliyopita katika siku kama ya leo, sawa na tarehe 4 Juni mwaka 1989, wanafunzi kadhaa wa vyuo vikuu vya China waliuawa na wengine wengi kujeruhiwa na polisi katika mji mkuu wa nchi hiyo Beijing. Siku hiyo maelefu ya wanafunzi wa vyuo vikuu vya China walikuwa wamejikusanya katika mzunguko wa Tiananmen mjini Beijing, wenye maana ya 'Amani ya Mbinguni" wakitaka kuwepo mazingira ya wazi ya kisiasa nchini humo, kupunguzwa uwezo wa chama cha kisoshalisti, kuongezwa uwezo wa bunge na kuchaguliwa wawakilishi wake. Ingawa serikali ya China ilipinga maandamano hayo lakini wanafunzi waliendela kukusanyika na mwishowe askari polisi na vikosi vya jeshi kutumia silaha kuwakandamiza wanafunzi hao waliokuwa wakiandamana ambapo baadhi waliuawa na kujeruhiwa.

No comments:

Post a Comment