Your help needed

As we committed ourselves to have our own premises for an improvement and to provide high quality of Islam education for the muslims in Leicester, Madrasatul Noor Leicester would like to take an oppertunity to inform every one who wish to contribute and to support our project to use our account below: Madrassatul Noor Leicester Lloyds TSB Bank Account number: 45127768 Sort Code: 30-94-97 International Bank account: LOYDGB21029 GB27LOYD30949745127768 If you would like to have more information please do not hasitate to contact us through these emails: madrasatulnoor.01@gmail.com or fcalwattan@gmail.com With a lot of thanks

26 Dec 2011

Hatupaswi kusheherekea mwaka mpya wa kikafiri


Imepokelewa toka kwa Abu Sa’iyd Al-Khudhriyy (RA) kwamba Mtume (SAW) amesema:
لَتَتَّبِعُنَّ سَنَنَ مَنْ قَبْلَكُمْ شِبْرًا بِشِبْرٍ وَذِرَاعًا بِذِرَاعٍ حَتَّى لَوْ سَلَكُوا جُحْرَ ضَبٍّ لَسَلَكْتُمُوهُ, قُلْنَا يَا رَسُولَ اللَّهِ, الْيَهُودَ وَالنَّصَارَى؟ قَال: فَمَنْ
“Mtafuata nyendo za watu waliokuwa kabla yenu, kiganja kwa kiganja, mkono kwa mkono, hata wakiingia kwenye shimo la kenge mtawafuata)). Tukasema: Ee Mjumbe wa Allaah, ‘Je, Unamaanisha Mayahudi na Manaswara?’ Akasema: Kwani nani zaidi ya wao?” [Al-Bukhaariy na Muslim]
Tunakaribia kuingia mwaka mpya wa Kikristo (wa kalenda ya Papa Gregory ijulikanayo kama ‘Gregorian Calendar’), na kuna Waislamu wengi tunaosherehekea mwaka huo mpya kama wanavyofanya makafiri, jambo ambalo halimo katika mafundisho ya dini yetu Kiislamu.

Imekuwa ni kawaida Waislamu kujiunga na wafanyakazi wenzetu, marafiki zetu au majirani zetu kusherehekea sherehe hizi potofu, na kuwa na tabia isiyoendana na mwenendo na mafundisho ya dini yetu tukufu. Hivyo tumeona ni muhimu tuwatumie ujumbe huu ndugu zetu popote walipo wajiepushe na mambo haya ya uzushi ya kuiga makafiri.

Swali ni kwamba, Vipi Muislamu ajitengee siku kama hizo na kusherehekea? 

Jibu kutoka kwa Mwanachuoni wa Ummah, Shaykhul Islaam Ibn Taymiyyah kwamba:
"Sisi Waislamu tusifanye jambo lolote lilokuwa si la kawaida katika siku hizi. Iwe kama siku yoyote nyingine katika maisha yetu bila ya kuwa imekhusishwa na lolote kama mfano wao watu wa Vitabu walivyokuwa hawasherehekei wala kuzifanya siku zetu za ‘Iyd kuwa ni khaswa (maalum) kwao."


Allah (SA) ametuonyesha ubaya wa makafiri katika aya nyingi kama hii ifuatayo:
إِنَّ الْكَافِرِينَ كَانُواْ لَكُمْ عَدُوًّا مُّبِينًا
Hakika makafiri ni maadui zenu walio wazi wazi.” [An-Nisaa: 101]
Vile vile Amewaita kuwa ni jamaa wa mashaytwaan na vikosi vyao.

Kuungana na Ahlul-Kitaab katika sherehe zao imekatazwa kama vile ilivyokatazwa kuungana na washirikina. Asibishe mtu kusema kuwa imemaanishwa ni washirikina peke yao na kwamba watu wa vitabu wana mielekeo au mila kama ya Waislamu takriban.

Shaykhul Islaam Ibn Taymiyyah ametoa dalili za kuharamishwa kusherehekea Krismasi, sherehe za wafursi kama Neyrouz, Sherehe za Mayahudi na nyinginezo (kama hizi za mwaka mpya) kwa kusema kwamba zote zinakuja katika hukumu hiyo hiyo moja.

Muislamu anapaswa kukataa mwaliko huo wa kusherehekea mwaka mpya hata kama mwaliko huo umetoka kwa Muislamu mwenzake.   


Mtume (SAW) ametukamilishia dini yetu kabla ya kufa kwake na ametujulisha kila jambo lililokuwa jema na ametukataza kila jambo lililokuwa baya. Kwa hiyo katika mafundisho yake ya Sunnah hakuna hata mwaka mmoja uliothibitika kwamba Maswahaba walisherehekea mwaka mpya unapoingia hata wa Kiislam sembuse huo wa kikafiri!

Katika Sunnah, Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ‘anhu) amesema:
‘‘Mtume (SAW) alikuja Madina na walikuwa wana siku mbili ambazo walikuwa wakipumzika na kustarehe pamoja na kucheza. Mtume akauliza: "Hizi ni siku gani?" Wakajibu: Ni siku ambazo tulikuwa tukicheza na kustarehe katika Ujaahiliya". Mtume (SAW) akawaambia: "Allaah Amekupeni zilizo bora kuliko hizo; Yawmul-Adhwhaa (‘Iydul-Adhwhaa) na Yawmul-Fitwr (‘Iydul-Fitr) )) [Abu Daawuud]

Hii inaonyesha dhahiri kwamba Mtume (SAW) ameharamisha Ummah wake kusherehekea sherehe za makafiri na amefanya hima kuzifuta kwa kila njia.

Sababu mojawapo ya kuharamishwa sherehe zao kama za mwaka mpya ni kwa sababu ya maovu, uchafu na fitna zinazotokea humo. Na hata kama hakuna maovu yanayotendeka humo lakini kusherehekea kutasababisha uzushi huu kuendelea katika vizazi vyetu na kusababisha kuingiza mila za kikafiri ndani ya Uislamu. 

Makafiri ni maadui wetu na maadui wa Allah (Subhaanahu wa Ta’ala) Kwa hiyo inatupasa tujiepushe nao kadiri tuwezavyo ila tu kwa yale tuliyoruhusiwa katika sheria ya Kiislamu. 

‘Umar Ibnul-Khatwtwaab amesema: "Jiepusheni na maadui wa Allaah katika sherehe zao"


Imeripotiwa katika mapokezi sahihi kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Amr akisema: “Yeyote anayeishi katika nchi isiyo ya Kiislam na akasherehekea sherehe yao ya mwaka mpya, na kuwaiga na akafa katika hali hiyo, basi atakusanywa pamoja nao siku ya Qiyaamah”.

Wa Allaahu A’alam

No comments:

Post a Comment