Baadhi ya Quran zilizokutwa zimechomwa moto
Takriban raia saba wa Afghanistan waliuwawa kwa kupigwa risasi na wengine wakajeruhiwa jana katika mapambano kati ya polisi na waandamanaji waliokuwa wakipinga kuchomwa moto Quran, katika kambi moja ya kijeshi ya Marekani.
Mjini Kabul na katika mikoa ya mashariki, kaskazini na kusini mwa mji huo mkuu wananchi wa Afghanistan waliojawa na hasira waliingia mitaani wakipiga kelele zilizosema "Kifo kwa Marekani" huku wakirusha mawe na kuchoma moto maduka na magari, na wakati huohuo milio ya risasi nayo ilisikika.
Katika mji wa mashariki wa Jalalabad, wanafunzi walichoma moto kibonzo cha Rais Barack Obama, huku ubalozi wa Marekani mjini Kabul ukifungwa.
Kamanda wa Marekani nchini Afghanistan, Jenerali John Allen, aliomba radhi kuhusiana na tukio la kuchomwa moto Quran na akaamuru uchunguzi wa kina ufanywe.
Bwana Allen na Naibu Waziri wa Ulinzi wa Marekani Ashton Carter walimwomba msamaha kwa Rais wa Afghanistan Hamid Karzai kwa tukio hilo lililotokea katika kambi ya wanajeshi wa angani iliyopo Bagram. Karzai alimtaka Allen kushirikiana kikamilifu katika uchunguzi wa serikali katika tukio hilo, na akamtaka ahakikishe kuwa matukio ya aina hiyo hayatokei tena.
Raia wa afghanistan wakionyesha kukasirishwa na kitendo cha uchomwaji wa Quran katika kambi moja ya kijeshi ya Marekani huko Afghanistan
Video:
No comments:
Post a Comment