As-Salaamu 'Alaykum wa RahmatuLLaah wa Barakaatuh
Tunapenda kuwaatarifu kwamba mwezi wa Dhul-Hijjah umeandama na hivyo siku ya Alkhamis ni mwezi 1 Dhul-Hijjah 1435 (25 Septemba 2014) na ‘Arafah itakuwa ni Siku ya Ijumaa mwezi 9 Dhul-Hijjah (3 Oktoba 2014) na ‘Eidul-Adhw-haa itakuwa ni Jumamosi mwezi 10 Dhul-Hijjah (4 Oktoba 2014)).
Kadhaalika tunapenda kuwakumbusha ndugu zetu mambo mawili muhimu tunayoghafilika nayo katika masiku ya Dhul-Hijjah
Kuchinja: Wenye kunuia kuchinja au kuchinjiwa, wanatakiwa wajizuie kukata nywele na kucha kuanzia unapoingia tu mwezi wa Dhul-Hijjah mpaka watakapomaliza kuchinja. Haya ni maamrisho yanayopatikana katika Hadiyth ifuatayo:
عن أم سلمة رضي الله عنها، أن النبي صلى الله عليه وسلم قال: (((ِذَا رَأَيْتُمْ هِلَالَ ذِي الْحِجَّةِ وَأَرَادَ أَحَدُكُمْ أَنْ يُضَحِّيَ ، فَلْيُمْسِكْ عَنْ شَعْرِهِ وَأَظْفَارِهِ))) وفي راوية: ((فَلَا يَأْخُذْ مِنْ شَعْرِهِ وَلَا مِنْ أَظْفَارِهِ شَيْئًا ، حَتَّى يُضَحِّيَ)) مسلم
Imetoka kwa Ummu Salamah (Radhiya Allaahu 'anha) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Ukiandama mwezi wa Dhul-Hijjah na ikiwa yuko anayetaka kuchinja basi azuie (asikate) nywele zake na kucha zake) Na katika riwaya nyingine ((Asikate nywele wala kucha mpaka akimaliza kuchinja)) [Muslim na wengineo]
Source: Alhidaaya