Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Mohammed
Gharib Bilal akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya SSB. Ndg.
Said Salim Bakressa.
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Dkt Mohammed Gharib Bilal akisalimiana na Rais Mstaaf
wa Tanzania Alhajj Ali Hassan Mwinyi,alipowasili viwanja vya Masjid Huda
Mbagala Chamazi kwa ajili ya Uzinduzi wa Masjid Huda.
Rais Mstaafu wa awamu ya
pili, Ali Hassan Mwinyi, akikata utepe kuzindua rasmi Msikiti wa ‘Masjidil
Huda’ uliojengwa na mfanyabiashara maarufu nchini, Said Salim Bakhresa
katika eneo la Uwanja wa Chamazi, Mbagala jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti huyo wa
Makampuni ya SSB, Said Salim Bakhresa, ambapo pia uzinduzi huo uliofanyika leo
Julai 4, 2014, ulihudhuriwa na baadhi ya Viongozi wa Kiserikali akiwemo na
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na
wengineo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (wa tatu kulia) Rais
Mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi (wa pili kushoto) Katibu Mkuu wa CCM
Abdulrahman Kinana ( wa pili kulia) Mwenyekiti wa Makampuni ya SSB, Said Salim
Bakhresa (katikati) na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum
(kushoto) wakijumuika na waumini wa dini ya Kiislam, wakati wa hafla ya
uzinduzi wa Mkititi wa ‘Masjid Huda’ na Swala ya Ijumaa uliofanyika leo Julai
4, 2014, Chamaz jijini Dar es Salaam.