Rais wa Ufaransa akipiga kura
Duru ya kwanza ya uchaguzi wa kuwania urais nchini Ufaransa iemanza hii leo kwa kuelekea wananchi katika masanduku ya kupigia kura.
Utata mkubwa katika uchaguzi huo ni kutoshiriki zoezi la kupiga kura watu ambao wametimiza masharti ya kupiga kura katika uchaguzi huo.
Taasisi za uchunguzi wa maoni zimeripoti kuwa asilimia 25 ya watu waliotimiza masharti ya kupiga kura, kuna uwezekano mkubwa wasipate fursa ya kushiriki katika uchaguzi huo.
Hivi sasa mashirika yanayojihusisha katika uchaguzi huo yamepigwa marufuku kutabiri au kutangaza matokeo ya uchaguzi huo kabla ya masaa 20 ya kutangazwa rasmi. Waledi wa mambo wanasema kuwa, wanatabiri kuwa Rais wa sasa wa Ufarans Nicola Sarkozy atashindwa na mpinzani wake wa chama cha Harakati ya Kitaifa Francois Hollande.
Wakati huo huo Waislamu waishio nchini Ufaransa wametangaza kuwa, hawatampigia kura rais wa sasa wa nchini hiyo kutokana na misimamo yake ya kiadui dhidi ya Waislamu na dini yao.
No comments:
Post a Comment