Mshukiwa mkuu wa ugaidi raia wa Ujerumani mwenye asili ya Uturuki ambaye amekuwa akisakwa na polisi ya Kenya kufuatia mripuko wa mwezi uliopita mjini Nairobi ametiwa mbaroni katika nchi jirani ya Tanzania.
Mwezi uliopita polisi ya Kenya ilitoa picha ya mwanamme mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Emrah Erdogan Mjerumani mwenye asili ya Uturuki ambaye pia anafahamika kwa jina Salahuddin al Kurdi.
Polisi ya Kenya imesema mshukiwa huyo wa ugaidi aliingia nchini humo mwezi Mei akitokea Somalia. Emrah Erdogan ambaye anatuhumiwa kuhusika na mripuko wa Nairobi ulioua mtu mmoja na kuwajeruhi wengine zaidi ya 30 hivi sasa anashikiliwa katika korokoro za polisi mjini Dar es Salaam Tanzania huku akiendelea kuhojiwa.
No comments:
Post a Comment