Baadhi ya watu waliohudhuria Khitma hiyo wakiwa nje ya jengo la Afisi Kuu ya CCM, Kisiwandui
Rais mstaafu wa Zanzibar Amaan Karume akiwasili katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM kuhudhuria khitma ya marehemu baba yake Abeid Karume
Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanziba Maalim Seif nae akiwasili viwanjani hapo
Makamu wa pili wa Rais Zanzibar, Balozi Ali Seif Iddi akisalimiana na baadhi ya viongozi wa chama
Mama Fatma Karume akisalimiana na kamishna wa Polisi Mussa Ali, alipowasili katika viwanja vya Kisiwandui kuhudhuria khitma ya aliyekuwa mumewe hayati Abeid Karume
Rais mstaafu wa Tanzania bwana Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na baadhi ya viongozi alipowasili viwanjani hapo
Rais wa Zanzibar Dokta Ali Mohamed Shein akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Chama na Serikali alipowasili uwanjani hapo
Waliohudhuria walisoma Quran na baadae kufatiwa dua
Baadae ilikuwa kumuombea marehemu dua katika kaburi lake. Mufti mkuu wa Zanzibar sheikh Omar Kabbi akisoma dua
No comments:
Post a Comment