Wimbi kubwa la malalamiko ya wananchi wa Afghanistan dhidi ya kitendo kiovu cha askari wa Marekani cha kuchoma moto Qur'ani Tukufu limewalazimisha wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa kuondoka nchini humo.
Ripoti zinasema Umoja wa Mataifa kama zilivyofanya taasisi nyingine za kimataifa, umelazimika kuwaondoa wafanyakazi wake nchini humo kwa sababu za kiusalama kutokana na machafuko na mapigano yaliyosababishwa na kitendo kiovu cha askari wa Marekani katika kituo cha anga cha Bagram cha kuchoma moto nakala za Qur'ani Tukufu.
Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wameondoka katika mji wa Kunduz huku waandamanaji wakijaribu kuvamia ofisi za taasisi hiyo ya kimataifa.
Maandamano na malalamiko ya wananchi wa Afghanistan dhidi ya kitendo hicho kiovu cha askari wa Marekani yangali yanaendelea licha ya kupita wiki moja tangu askari hao wachome moto nakala za kitabu hicho kitakatifu.
No comments:
Post a Comment