Kijana wa Mauritania ambaye bado damu yake inaendelea kuchemka na bado ni nguvu kazi ya Taifa,ameamua kujiwasha moto ili afe mbele ya jengo la Baraza la Seneti la Mauritania karibu na lango kuu la Ikulu ya Rais katikati ya mji mkuu wa Mauritani, Nouakchott-jioni ya siku ya Alhamisi.
Walinzi wa Ikulu ya Rais, waliingilia kati na kuanza kuuzima moto na kumkimbiza Hospitalini,akiwa bado yuko hai.
Mpaka sasa haijulikana afya ya kijana huyu huko Hospitalini na hata sababu iliyopelekea kijana huyu ajichome moto bado haijajulikana.Ispokuwa baadhi ya vyanzo vya habari vimesema kwamba:
Kijana huyu ni mmoja kati ya wale waliobeba vyeti vya wasiokuwa na kazi au wasiokuwa na ajira na ambao walitishia hapo mwanzo kuwa ikiwa hawatozingatiwa na kupata ajira basi watajichoma moto wenyewe,na hii ilikuwa ni baada ya kuvichoma moto vyeti vyao vya kielimu kutokana na kukata tamaa.
Tukio hili ni la aina yake kutokea nchini Mauritania tangu kijana mwingine aliyeitwa Yaqub mtoto wa Dahud kujichoma moto mwenyewe mwaka uliopita katika sehemu hiyo hiyo alipokijana huyu akiungua moto kama anavyoonekana kwenye picha.
No comments:
Post a Comment